HISTORIA

Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar ilianzishwa  February, mwaka 2018 kutokana na matakwa ya Sheria kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984 Toleo la 2010 chini ya kifungu Kifungu 42(1) inayompa Rais wa Zanzibar kuunda au kuanzisha taasisi kadri atakavyoona inafaa. Wizara ya Vijana ni miongoni mwa Taasisi muhimu sana kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na majukumu iliopangiwa na Serikali likiwemo suala la kuratibu na kuwaunganisha vijana katika masuala ya Michezo na Sanaa, ili kutimiza Malengo ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ya kuimarisha Michezo, utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 pamoja na kufikia Malengo ya kuwainua vijana ili kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa Kukuza Uchumi na kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA).

Wizara ya Vijana ni miongoni mwa Taasisi muhimu sana kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na majukumu iliopangiwa na Serikali likiwemo suala la kuratibu na kuwaunganisha vijana katika masuala ya Michezo na Sanaa, ilikutimiza Malengo ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ya kuimarisha Michezo, utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 pamoja na kufikia Malengo ya kuwainua vijana ili kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa Kukuza Uchumi na kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA).

Kimajukumu Wizara ya Vijana imepangiwa kusimamia na kuratibu shughuli za Uendeshaji na Utumishi; kuratibu Mipango, Sera na Utafiti;  Kusimamia masuala yote yanahusu sekta ya Vijana, sekta ya Utamaduni, sekta ya Sanaa na sekta ya Michezo. Aidha, Wizara hii ina jukumu la kuratibu shughuli za kukiendeleza Kiswahili kupitia BAKIZA na Kusimamia haki za Wasanii kwa kupitia Idara yake ya COSOZA.

Katika marekebisho ya Wizara za Serikali yaliyofanyika mwaka 2018 Idara ya Michezo na Idara ya Utamaduni na Sanaa zilihamishwa kutoka Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale. Wakati Baraza la Vijana na Idara ya Maendeleo ya Vijana nazo zilitoka Wizara ya Wanawake na Watoto,  na kitengo cha Hakimiliki kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa pamoja kuunda Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa uwezo aliopewa Mh. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa Kifungu 42(1) cha Katiba ya Mwaka 1984, na kukabidhiwa majukumu ya kusimamia na kuendeleza Sekta za Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

 Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa, Muundo huu ni muhimu kwa Wizara na Taasisi zake katika kufanya kazi kwa dhamira iliyokusudiwa na kutoa matokeo chanya yanayotarajiwa kwa Umma.