HUDUMA ZETU

HUDUMA MAHSUSI YA WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO.

 1. Kusimamia uendelezaji na uimrishaji wa sekta ya michezo pamoja na miundombinu kwa maendeleo ya michezo;
 2. Kusimamia na kuendeleza mabaraza ya vijana wa lengo na maslahi mapana ya kuwaunganisha vijana katika taifa na kuongeza tija kwao.
 3. Kuratibu masuala ya utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa katika kupitisha zabuni za utekelezaji wa miradi ya Wizara.
 4. Kukusanya mapato na kufanya malipo ya huduma zinazotolewa katika baadhi ya Taasisi kama vile studio ya muziki.
 5. Kuboresha maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii.
 6. Kuratibu uibuaji wa miradi, ufuatiliaji na tadhmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
 7. Kutoa ushauri wa kitaalamu katika masuala mbalimbali yakiwemo ya maendeleo ya vijana, maendeleo ya utamaduni na sanaa na pia maendeleo ya michezo.
 8. Kusimamia utekelezaji washeria za nchi ambazo zinasimamiwa na Wizara ya vijana ,Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na sheria ndogo ndogo zinazotungwa chini ya sheria hizo.

VIWANGO VYA HUDUMA ZETU

Viwango vya mahusiano.

Tunaendeleza mahusiano mazuri na wateja wetu kwa kutekeleza yafuatayo:-

 • Tutatoa kipaumbele kwa watu wenye mahitaji maalum.
 • Tutatoa huduma za kitaalam kwa ufanisi na muda muafaka.
 • Tutatoa huduma kwa uwazi , nidhamu, usawa na bila ya upendeleo.
 • Tutatoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na huduma zetu.
 • Tutatoa ushiriiano katika kupanga na kufanya maamuzi.
 • Tutatoa taarifa sahihi za uhakika kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka.