MICHEZO

BARAZA LA TAIFA LA MICHEZO LA ZANZIBAR

Majukumu ya Baraza la Taifa la Michezo : Baraza la Taifa la Zanzibar lina jukumu la kukuza na uendeleza michezo nchini pamoja na kuifanya Zanzibar kuwa ni kituo kwa wanamichezo.

Ahadi za Baraza la Taifa la Michezo

  1. Tutaendeleza, tutastawisha na kudhibiti aina zote za Michezo katika Wilaya kwa ushirikiano wa Vyama vya Michezo vya Wilaya vilivyosajiliwa kwa kila siku.
  2. Tutatoa mafunzo kwa viongozi, wachezaji, walimu , waamuzi na madaktari wa tiba ya michezo katika ngazi ya wilaya kila itapohitahitajika.
  3. Tutatoa misaada ya kisheria na kikanuni kwa vilabu na vyama vya Michezo vya Wilaya vilivyosajiliwa kila itakapohitajika.
  4. Tutahamasisha wananchi kwa ujumla wao wa vyama vya Michezo vya Wilaya na kusaidia kuhifadhi uvamizi wa viwanja vya michezo kwa kushirikiana na Afisi ya Mkuu wa Wilaya husika kwa kila baada ya miezi mitatu (3)
  5. Tutasaidia kuandaa taratibu za kuvisaidia vilabu na vyama katika kupata misaada kama vile vifaa vya michezo ambavyo ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza michezo Wilayani pale itakapoonekana inafaa kufanya hivyo kila itakapohitajika.
  6. Tutatoa fursa za ushirikiano miongoni mwa vyama vya michezo mbali mbali vya wilaya kila siku.
  7. Tutaidhinisha na kuthibitisha mashindano na matamasha katika michezo inayoandaliwa na vyama vya Michezo vya Wilaya kwa wakati.
  8. Baada ya kushauriana na vyama vya michezo vya wilaya tutaandaa mashindano na/au Matamasha ya wilaya kwa nia ya kubadilishana uzoefu na kukuza uhusiano wa kiafrika miongoni mwa wana michezo kila itakapobidi kufanya hivyo.
  9. Tutatekeleza Sera ya Taifa ya maendeleo ya michezo kila siku.