UTAMADUNI NA SANAA

BARAZA LA SANAA , SENSA YA FILAMU NA UTAMADUNI (BASSFU)

Majukumu ya Baraza la Sanaa Sensa ya Filamu na Utamaduni:

Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni lina jukumu la kukuza kusimamia na kuendeleza shughuli za sanaa, muziki na Utamaduni pamoja na kuifanya Zanzibar kuwa kivutio cha wageni kwa kusoma Utamaduni wa Zanzibar.

Ahadi za Baraza la Sanaa Sensa ya Filamu na Utamaduni.

 1. Tutavitambua na kuvisajili vikundi vyote vya sanaa na vyama vya sanaa vilivyopo Zanzibar kila siku.
 2. Tutatoa muongozo wa jumla kwa kamati za sanaa na sensa ya filamu za wilaya juua ya maonesho yanayofanywa katika majukwaa na burudani nyenginezo kila inapohitajika kufanya hivyo.
 3. Tutahakikisha filamu zote zilizorikodiwa nje ya Zanzibar ziwe zenje kuzingatia Utamaduni na silka za nchi kwa lengo la kuoneshwa hadharani kila siku.
 4. Tutakagua matangazo ya burudani yanayotolewa kwenye magari na mabango ya biashara kwa kila mwezi.
 5. Tutathibitisha maombi kwa vikundi vya wasanii kutoka nje ya Zanzibar vinavyotaka kufanya shughuli zao Zanzibar kila itakapohitajika.

KAMISHENI YA UTAMADUNI NA SANAA

Majukumu ya Kamisheni ya Utamaduni na Sanaa:

Kamisheni ya Utamaduni na Sanaa ina jukumu la kukuza,kusimamia, na kuendeleza shughuli za sanaa , na Utamaduni pamoja na kuifanya Zanzibar kuwa kivutio cha wageni kwa kusoma utamaduni wa Zanzibar.

Ahadi za Kamisheni ya Utamaduni na Sanaa.

 1. Tutahifadhi , tutalinda na tutaimarisha mila , silka na maadili ya Utamaduni wa Zanzibar kila siku.
 2. Tutalinda sera ya taifa katika mambo yanayohusu sanaa na Utamaduni na kuitangaza sera hiyo kila siku.
 3. Tutasaidia ushiriki wa kikundi au mtu binafsi katika kuwakilisha Zanzibar katika shughuli za sanaa ndani au nje ya Zanzibar kila itakapohitajika.
 4. Tutashughulikia na kuwezesha utafiti katika maendeleo na uzalishaji wa kazi za sanaa Zanzibar kila baada ya miezi sita (6).
 5. Tutasimamia na tutaandaa taratibu na kuwapatia zawadi kitaifa wasanii waliotoa mchango wao kwa taifa kwa kila mwaka.
 6. Tutaimarisha sanaa ya ndani na maonesho ya kitaifa na kimataifa na tutasaidia mafunzo , utafiti na uenezaji kila itakapohitajika.